RIWAYA; MATESO YA KISASI
MTUNZI; DANPHORD S. CHILUMBA
SIMU; 0758 145320
E MAIL; danchilumba34@gmail.com


i



Ilipoishia....


 Mzee Chisa ni miomgomi mwa mafundi ujenzi mahiri na maarufu sana katika jiji la Dar es salaam, mzee huyu alikua akiishi maeneo ya kibera pembezoni mwa jiji la Dar es salaam. Akiwa ndani na mke mdogo bi Alfan ghafla alisikia hodi nje,wakati hou mvua kubwa sana ilikua ikiendelea kunyesha huku miungurumo ya radi ilioambata na miale ya hapa na pale ikiwaka, bila kuacha nyuma miungurumo ya kutisha ikiendelea.
Mvua kubwa iliendelea kummiminikia mwilini mama yake Edwini huku akiendelea kubisha hodi mlangoni mwa Mzee Chisa,
"Hooodiii..... Hodiiii" Mama Edwini aliendelea kuita
"Hooodiii wenyewe humu ndanii..." Mama Edwini aliendelea kuita kwa bidii.


ENDELEA....


" Mama Edwin?" Mzee chisa alishangaa kumuona mama Edwin akiwa nyumbani kwake saa hizo huku akiwa amelowana mwilini mzima kutokana mvua kubwa iliomnyesshea.
"Habari baba Edwin?" alisalimia mama Edwin
kambla ya kujibu salamu baba Edwin alimshambulia na maneno makari sana
"We mwanamke vip, una shida gani na umefuata nini saa hizi tena na mvua hii?"
Mama Edwin akiwa  anajiuliza aanze kujibu swari lipi kati ya yale alioulizwa na mume wake huyo alieamua kuiacha familia na kwenda kuishi na mke wa pili na kuwa telekeza watoto katika maisha yasioeleweka.
"Hapana baba Edwin......."
kabla hajaendelea na utetezi wake....
                                       **********************************

"Edwin...." Mwalimu alimuita Edwin
Huku akiwa anatetemeka mwili mzima Edwin alimuitikia mwalimu wake na kumsikiliza kwa msisitizo huku akiwa anamwangalia usoni kwa uso uliojaa wasiwasi mwingi usiofichika.
"mwenzako yuko wapi?" aliuliza mwalimu Jerry
"mmmh.... nmh... sijuuu... sijuiiii mwalimu..." huku Edwini akiwa ni mwenye hofu akijibu swari hilo.
"Hujui?" aliuliza mwalimu Jerry huku akionekana ni mtu mwenye ghadhabu dhahiri.
"wewe kidume unaejua kutongoza harafu usijuie unaemt*** yuko wapi mpaka muda huu?"
kwa maswari na msisitizo aliouonesha mwalimu Jerry kwa awamu hii ilizidi kumpa hofu Edwin na kujikuta akiwa anakosa ujasiri na kuanza kutirirka jasho lisilokua na kificho.
"nakupa dk chache unatakiwa uje na huyo mpumbavu mwenzio haapa...sawa?"
akiwa bado ni mwenye hofu aliitikia kwa kichwa
                               *********************************************

Alitoka bibi Alfan ndani na kuanza kumtolea maneno makali mama Edwin na yenye kashfa pamoja na matusi.
Pasipo kusikilizwa hata alikuja na shida gani kwa wakati huo, mvua ikiwa bado inaendelea kumiminikia mwilini mwake.

Mama Edwini aliingiwa na maumivu sana moyoni mwake na kuanza kuongea kwa kwikwi, laiti kama kungekua hakuna mvua kwa wakati ule basi machozi yaliokua yanamtoka kama maji yangeonekana dhahiri. lakini machozi hayakuweza kuonekana kwa kua mvua kubwa ilikua ikimmiminikia.

"Hivi wewe mama Edwinin huna haya?" alidakia Mzee Chisa kabla hata mama Edwin hajaongea chochote

swari hilo lilimpa nguvu ya kujikaza na kuanza kuporosha maneno mfululizo
"hivi weee mwanamme ni wsa aina gani?? kweli we ni mwanamme kweli??"huku akiwa amefura kwa hasira, akamgeukia mke mwenza na kuanza kumpasha yake.
"Weee mwanamke hivi hujui kama huyu ni mme wangu wa ndoa?, onesha kitu kama hiki..." akiwa anamwonesha mkono wa kushoto katika kidole cha kati kilichovishwa pete ya ndoa iliyovikwa na mumewe huyo pindi walipokula kiapo cha upendo kanisani miaka kadhaa iliopita.
"Nina familia nae mimi, huyu ni mume wangu hata kwa mbele za haki najulikan, weewe unajulikana? mala*** weee..." aliendelea kufoka mama Edwin
"Sijaja hapa kuomba ugali wala hifdhi yoyote, bali nimekuja kumshirikisha maendeleo ya matunda yetu tuliovuna kwenyhe ndoa.." aaaakamgeukuia Mzee Chisa "mwanao anaumwa na yupo hoi mahututi." akageuka na kuamua kuondoka eneo hilo ili kuepusha hali ya hewa kuendelea kuchafuka au mambo mengine kutokea zaidi.
 Maneno haya ya mke wake huyo mama Edwin yalimfanya kuwa katika hali fulani, na kuanza kukumbuka kitu..
                                       ******************************************
Ni kumbukukumbu za nyuma ambazo Edwini alikua anajaribu kukumbuka akiwa ndani baada ya kurud shule , na kumbukumbu hizi zilikua zikimniyima  raha kabisa. kwa maana tangu kipindi hicho ambacho Edwin alimwandikia barua na barua hiyo kukamatwa na mwalimu Jerry, Konsolata hakuendelea tena na masomo aliiacha shule.
"Aaaah.... basi bwana, sina kosa maana sikutaka yeye ache shule ila kama kaaamua sawa."
alijisemea kimoyomoyo Edwin
Ghafla aliingia mama yake akiwa amelowana chapachapa mwili mzima,
"Hee... vipi mama mbona hivyoo..."

ITAENDELEA.......

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii