
Riwaya: MATESO YA KISASI Mtunzi: Danphord S Chilumba Simu: 0758 145320 barua pepe: danchilumba34@gmail.com Sehemu 1 Ilikua asubuhi ya majira ya saa nne na dakika arobaini na tano (10:45) wakati huo wanafunzi wakiwa katika kipindi cha mapumziko, katika sehemu mbalimbali wakiendelea kupata chochote kitu ili kuweza kusaidia matumbo yao yahimili mikikiimikii ya masomo yaliyokua yakiendelea katika ratiba ya siku hiyo. Ni siku ambayo Edwini hatoisahau, kwa maana ni siku ambayo alimsababishia binti mmoja alieitwa Konsolata ambae nae pia alikua mwanafunzi wa darasa la nne kama alivyo Edwini kuweza kuacha shule. Ni baada ya mwalimu Jerry kukamata barua ya kimapenzi ambayo Edwini alimwamdikia Konsolata, hivyo mwalimu Jerry baada ya kuletewa barua hiyo na mmoja wa wanafunzi wa darasa hilohilo la nne ambae ni fatma, ni baada ya EDdwini kuandika hiyo barua na kuiifadhi ndani ya daftari la kiswahili ili baadae amkabidhi Konsolata. baahati mbaya barua ilidondoka na Fatma al...